Top Ad 728x90

Friday 26 February 2016

Watoto Wawili Wamshtaki Mahakamani Mchungaji TB Joshua Kwa Kifo Cha Baba yao..Wadai Fidia ya Dola $521,000


Watoto wawili wa Afrika Kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii Ayorinde ameiambia BBC.

Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na mwingine wa miaka sita wamewasilisha nyaraka za mashtaka katika mahakama ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos, wakidai fidia ya zaidi ya dola $521,000; kutoka kanisa la Synagogue Church of All Nations, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti.

Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekuwa wakisisitiza kwamba hawana kosa lolote
Baba yao alikua miongoni mwa watu 116 waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014.

Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo, akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90