Imevuja!
Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi
filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa
ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa
kutosha!
Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa
hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa
Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka
kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi.
Giggy Money
NCHI ZENYE WATEJA WENGI
Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi
ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini.
India ni kwa mbali sana!
INAVYOKUWA SASA
Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye
mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya
‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume
wakiwaona wavutike haraka.
“Baada ya wanaume wateja kuziona picha zetu kwenye Instagram na
kuvutiwa, sasa hutaka kuwasiliana kwa kutumia Insta Direct (mawasiliano
ya wawili tu ‘in box’).
“Hapo sasa ndiyo huwa pazuri, kwani kama mwanaume atakuwa amekolea,
atatangaza dau na kumtaka staa aliyempenda amfuate nchini mwake. Kama ni
Dubai, China au Afrika Kusini,” kilisema chanzo hicho.
Kidoa
UJIRA WAO
Chanzo hicho kilisema kuwa, ujira wanaolipwa mastaa hao ni wa chini sana
ukilinganisha na kiwango cha muda.“Mara nyingi kama ni Dubai,
unatangaziwa dola za Marekani 3,000 (kama shilingi milioni 6) ambapo
ndani ya humo ni pamoja na tiketi yako ya ndege kwenda na kurudi, malazi
ya kule kwa maana ya kukaa hotelini na kula.
“Siku ukirudi unapewa labda dola 500 tu ambazo ni kama shilingi milioni
moja na kidogo. Sasa hizo, ndiyo utaingia madukani kufanya manunuzi
mbalimbali ya vitu kama pafyumu, losheni, nguo na viatu. Ndiyo maana
masta wengi wakienda nje ya nchi kwa wanaume hurudi na mabegi ya vitu
walivyonunua.” Chanzo.
Jackline Wolper
HUWA WANAJAZA NAFASI
Katika hali ambayo ilishtua, staa huyo alisema kuwa, kwa tabia hiyo ya
kujiuza nchi mbalimbali, baadhi ya mastaa hujikuta nafasi zimejaa!
“Utakuta staa anatakiwa kwenda Dubai mwezi huu. Mwezi ujao anakwenda
China kwa mwanaume mwingine, akitoka China, Afrika Kusini mwezi Aprili.
Akitokea mwanaume akamtaka aende Dubai anakuta nafasi imejaa. Pengine
mpaka Mei.
“Mkifuatilia sana mtagundua ni kwa nini baadhi ya yetu hatutulii
nyumbani Bongo wakati hatuna biashara kusema ndiyo inatufanya tusafiri
kila wakati. Ni kujiuza tu! Mh! Mbona Instagram ina mambo!”
SIFA ZAO
“Tena nataka kukuongezea kwamba, ogopa sana mastaa ambao picha zao
kwenye Instagram ni za nusu utupu! Hebu we fikiria, Instagram mimi sioni
kama ni sehemu ya siri, sasa kwa nini mtu apige picha chafu halafu
azitupie kule, anatafuta nini? Maana hata baba yako, mama yako, ndugu
zako wanaweza kuona,” alisema staa huyo.
MASOGANGE ALITAJWA
Madai hayo yananyemeleana kwa karibu na habari iliyowahi kuandikwa na
Gazeti la Ijumaa la Januari 23, 2015 ikiwa na kichwa kisemacho;
MASOGANGE AIBU TUPU SAUZI
Habari hiyo ilimhusu modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Habari hiyo ilisema Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.
“Kimsingi hana kazi huku Sauz zaidi ya kuposti picha kwenye Mtandao wa
Instagram na anachanganya sana wanaume wenye pesa zao. Si unajua tena
mtoto kajaliwa shepu la maana. Ukitaka kuthibitisha hilo ingia katika
akaunti yake utaona picha kibao za kihasara akiwa hotelini.”
Hata hivyo, staa huyo alikuja kukanusha kuhusu picha zake na kujiuza huko bondeni ambapo alisema:
“Mie sijui hizo picha zilisambaa vipi sababu zilikuwepo kwenye kamera
yangu na mimi siku hiyo nilikuwa nimelewa. Sikuwa naelewa chochote na
nilikuwa South Africa (Afrika Kusini). Kwa hiyo masuala ya kuandikwa
kwamba nilikwenda kujiuza si kweli.”
KIDOA HIVI KARIBUNI
Hivi karibuni, video queen wa Bongo anayekuja kwa kasi, Asha Salum
‘Kidoa’ naye alisafiri kwenda Dubai akisema amepata dili. Lakini
hakuweka wazi ni dili gani kiasi kwamba, katika toleo moja la gazeti
ndugu na hili, Ijumaa liliandikwa makala yenye kichwa kisemacho; Kidoa;
Dubai umeenda kula bata, kujiuza au dili za ‘sembe’? Katika makala hayo,
mwandishi alitilia shaka baada ya kuona picha kwenye Instagram yake
zikimuonesha msanii huyo akiwa Dubai akila bata kwenye klabu ya hoteli
kubwa.
Wengi baada ya kuona binti huyo yuko Dubai walianza kujiuliza maswali
mengi. Kwamba kaenda kujipumzisha na kula bata au kaenda kujiuza kama
ambavyo baadhi ya mastaa wamekuwa wakifanya au ameanza kutumika katika
kusafirisha ‘sembe’? yaani unga au madawa ya kulevya.
Mwandishi alisema anaandika hayo kwa sababu anajua Kidoa hana mkwanja wa kusema anakwenda kupumzisha akili Dubai.
WENGINE HUWAUZA WENZAO
Katika maelezo mengine ya staa huyo, baadhi ya mastaa hao wanapokuwa nje
ya nchi na wanaume wao wa kwenye Instagram hugeuka na kuwa mawakala wa
kuwauza wengine.
“Lakini pia staa anaweza kuwa mfano, Dubai halafu akakutana na staa
mwenzake anakwenda mfano China, na yeye anakuwa wakala. Mimi niliwahi
kukutana na staa mmoja Dubai, anakwenda China, nikampa namba za simu za
mwanaume niliyewahi kuwa naye kule.
“Alipofika alimpigia, akamwambia amepewa namba na mimi, basi na mimi
nikalipwa changu maana nimemtafutia soko,” alisema staa huyo.
0 comments:
Post a Comment