Top Ad 728x90

Friday 26 February 2016

Diva Loveness Ahusishwa Katika Utapeli wa Kudhulumu Mtoto Kilema Aliyechangiwa na Wadau Kupitia Kipindi Chake


Diva Amejikuta Katika wakati mgumu baada ya Dada mmoja anajiita Ms_Resty huko instagram kumrushia shutuma za kung'ang'ania shilingi laki saba za msaada zilizochangwa na watu kumsaidia mtoto kilema kupitia kipindi cha Ala za roho cha anachokiendesha radioni...
Mpaka sasa Diva hajasema chochote kuhusu tuhuma hizi alizoangushiwa...

Dada huyu amepost hivi...

From @Ms_Resty - Jamani jamani Loveness Loveness aka Diva the bawse mbona hauendani na jina lako linalomaanisha Upendo??? Huu sio Upendo kumsaidia mtu haimniishi ndo uchukue pesa zake!!! Kumsaidia mtu haimanishii ndo umuonee kwa vile wewe ndo ulimtangaza kwenye kipindi chako! Anyway sijawai kuwa na mazoea na huyu dada ila kuna siku nilisikilizaga kipindi chake nikamsikia anamtangaza yule mama ambaye alikuwa na mtoto hana haja kubwa wala mguu mmoja nikaguswa kwa vile mimi pia nilishaakaga maeneo ya kawe nikaend kumuona nikampost apa Insta kumuombea msaada watu wakanisaidia kupost na wengine kutuma michango mbalimbali! Pesa ni pesa jamani mi sikutaga kukaa nazo ndo maana nikaweka namba yake hata wale baadhi walionitumia nilizituma pale pale kuepusha kuzitumia! Jamani sasa Diva wa Clouds @divathebawse kipindi cha Ala Za Roho ambaye ndo alimtangaza akwambia ampe pesa zote alizochangiwa ili yeye ndo awe anampatia kdg kdg huyo Mama Husna mama husna akumpa zote sababu nyingine tulizitenga ili tuulipie ule mguu wa mtoto akampa laki 7 akamwambia kwa vile yeye anafoundation na hayupo mwenyewe ndani ya iyo foundation atakuwa anampa kdg kdg anunue vifaa vya mtoto! Vifaa vimeisha Diva hataki kutoa pesa anasema huyo mama kamuongelesha vibaya na yeye ndo aliyemtangaza so itatumika kwenye charity nyingine! Sikumuelewa kabisa nikamwambia basi mimi namuombea msamaha huyu mama kama alimkosea ila pesa ampatie Diva kagoma! Hii sio sawa ni uonevu kumbuka baada ya mimi kupost ndo ilicreate Big awareness kwa watu wengine wakachanga sasa atachukuaje pesa za michango ya mtoto mlemavu mwenye matatizo agome kurudisha naombeni msaada jamani ubinadamu kazi! Na siku zote tenda wema uende zako! Hata angepata ngapi mwache apatemaana kumlea yule mtoto jamani sio lelemama!! Naombeni Diva atoe pesa nimemuomba ikashindikana na ndo maana nikaamua kuipost uku-Ms_Resty

My Take:
Ni vizuri Diva ajitokeze na kujibu tuhuma hizi ambazo zinazidi kusambaa mitandaoni...

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90