Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa kushirikiana na wamiliki wa
vyombo vya usafiri Dar es salaam wametangaza kuanzisha mpango wa
kuwasaidia Walimu wa Shule za Serikali kwa kuwapatia huduma za usafiri
bure katika daladala.
Akieleza mbele ya waandishi wa habari Makonda amesema ‘Nilianza kuongea na vyama vya usafirishaji kisha kujenga hoja dhidi ya changamoto za Walimu wetu, na nikawaomba viongozi hao tuonane kulijadili hili na kisha tukafika muafaka ’
‘Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam’
‘Tumeweka utaratibu, Walimu watalazimika kutengenezewa vitambulisho maalum ambavyo kila Shule itatengeneza vitambulisho vyake, huku kukiwa na mambo manne ya kuzingatia ambayo ni 1. Picha ya Mwalimu husika, 2. Jina la shule 3. Namba ya Mkuu wake wa shule 4. Kuwe na sahihi ya Mkuu wa Wilaya Paul Makonda’

0 comments:
Post a Comment