Top Ad 728x90

Monday 22 February 2016

Kisa Nicki Minaj, Shilole Asaka Ticha wa Kizungu Adai Hali ni Mbaya...


Kwenye ukurasa wake wa Instagram Shilole amendika tangazo akimtaka mtu ambaye ni mwalimu wa lugha hiyo kuwasiliana, ili aweze kuanza mafunzo hayo.

"Anatafutwa mwalimu wa kingereza mzuri, jamani huu sio utani nipo sirias naona hali ishakuwa sio hali soon natakiwa kuonaa na Niki Minaji hivyo lazima nijinoeee, namba ya sm 0653883839", aliandika Shilole kwenye ukurasa wake wa instagram

Shilole anafahamika kwa kutojua lugha ya kingereza, hivyo kuwa gumzo anapoongea lugha hiyo ambayo mara kwa mara huwa anachapia, lakini cha ajabu yeye mwenyewe huwa anafurahia na hajutii kuzungumza lugha hiyo ambayo haijui, kama alivyowahi kutamka neno la "I love is my country", ambalo lilikuwa maarufu na watu kuvutiwa nalo.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90