Top Ad 728x90

Wednesday, 24 February 2016

KIMENUKA...Mabilioni ya NSSF Yatafunwa


BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Tija la Taifa (NIP) imeishauri serikali kuunda tume ya kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali zaidi ya dola za Kimarekani 1.5 bilioni,anaandika Josephat Isango.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka 2012/13, imebaini kiasi cha dola za kimarekani 1,532,458.91 zilizotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zimetumika kinyume na taratibu za kisheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Samweli Wangwe, Mwenyekiti wa NIP, amesema kuwa, fedha hizo zilikua za   mkopo kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la Maarifa lililopo mtaa wa Ohio na Hollis jijini Dar es Salaam ambalo linamilikiwa na Shirika hilo zilipo.

Amesema, ripoti hiyo ilionyesha kuwa, kiasi cha dola za kimarekani 480,000 zilitumika kuilipa kampuni ya Zawadi Communication Limited ambayo inamilikiwa na Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), kama gharama za udalali wa kuitafutia NIP mbia wa ujenzi wa jengo hilo ambao ni NSSF.

Ameongeza kuwa, mashirika hayo mawili ni mali ya serikali, hivyo basi hakukuwa na ulazima wa kumtafuta dalali wakati makatibu wakuu wangeweza kukaa pamoja na kujadiliana namna ya kuweza kuingia makubaliano ya mkopo huo.

Amesema, licha ya kufanyika kwa malipo hayo, lakini ripoti hiyo imeonyesha kuwa, NIP haikuitisha zabuni yoyote ya kutafuta kampuni‎ ya udalali ya kutafuta mbia, jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Alisema Kutokana na hali hiyo, bodi hiyo ilipata mashaka juu ya malipo hayo na kuitaka serikali kuchunguza mwenendo mzima wa malipo hayo kama ulifuata taratibu za kisheria.

“NIP haikutangaza zabuni yoyote ya kutafuta kampuni ya udalali kwa ajili ya kutafuta mbia,lakini malipo yameonyesha kuwa, kampuni hiyo ililipwa kiasi hicho Juni16 mwaka 2011,jambo ambalo ni kinyume na sheria,” amesema Profesa Wangwe.

Amesema, licha ya malipo hayo kufanyika, lakini pia kiasi cha dola 831,214.48 zimebainika kutumika kinyume na sheria wakati ujenzi wa jengo hilo haujaanza kinyume na makubaliano ya mkataba wa mkopo huo.

Wangwe aiwambia waandishi kuwa bodi hiyo pia ilibaini kuwa, fedha zote ambazo ni dola 1,532,458,91 ziliingizwa Katika akaunti ya NIP kwa mkupuo moja wakati makubaliano yalikuwa ni kuingiza kwa awamu kulingana na mahitaji halisi.

“Kutokana na hali hiyo, NIP inatakiwa kulipa jumla ya dola 1,002,228.13 ambayo ni pamoja na riba ya asilimia 13.08 kwa kipindi chote cha miaka mitano, jambo ambalo linazidi kuitia hasara serikali,” amesema.

Alifafanua kuwa, mpaka sasa shirika hilo halina vyombo vya usafiri, badala yake viongozi wakuu akiwamo Mkurugenzi anakodisha gari lake binafsi kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Profesa Wangwe amesema kuwa, licha mkataba huo kuonyesha matumizi ya fedha hizo ambayo ni pamoja na kulipa gharama za wapangaji za kutafuta sehemu nyingine ili kupisha ujenzi huo pamoja na NIP kukodi ofisi wakati ujenzi huo unaendelea, lakini fedha hizo zimetumika kinyume na makusudio.

Amesema baada ya kubaini upungufu huo, bodi hiyo iliitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti kuhusu suala hilo ambao na wenyewe walikiri kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba huo kwenye matumizi ya fedha hizo.

Wangwe amesema kutokana na hali hiyo, bodi hiyo iliwasilisha mapendekezo ya kuitaka serikali kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Shirika hilo, Joel Mlanzi ambaye tayari ameshasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa suala hilo.

Chanzo: Mwanahalisionline

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90