Top Ad 728x90

Tuesday 23 February 2016

Ray C Aeleza Jinsi Magazeti ya Udaku yanavyo Mliza Mama yake


Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema mama yake amekuwa akipatwa na presha mara kwa mara kutokana na habari anazo ziona kwenye magazeti ya udaku kuwa mwanae amerudia matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television, Ray C amesema mama yake hana amani kutokana na mambo yanayo andikwa kwenye magazeti ya udaku.

“Mimi naweza nikasema nakushtaki, wewe una hela zaidi na unaweza ukanishinda, your powerful get a gun watu wanifyatue na wampige mama yangu, maana mama yangu yupo hospitali ana presha kwa sababu ya gazeti yake,” alisema Ray.

Wiki chache zilizopita gazeti la Ijumaa liliandika habari kuwa mwanadada huyo alionekama mazingira fulani ambayo yanadaiwa kupatikana madawa ya kulevya.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90