Top Ad 728x90

Wednesday 24 February 2016

HALIMA MDEE Afunguka...'Hakuna Ufisadi Uliofanyika Kwa Bahati Mbaya Bila ya Mawaziri na Wakurugenzi '


Mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es Salaama katika kwa tiketi ya Chadema, Mh. Halima Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna ufisadi ambao umefanyika nchini kwa bahati mbaya.

Mdee amesema kuwa kila ufisadi uliofanyika viongozi wa serikali walikuwa wakitambua sababu kuna muda mwingine walipokea memo kutoka katika uongozi wa juu ya nchi.

Halima Mdee amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Kawe na kusema kuna wakati wakurugenzi walikuwa wanapewa vimemo kutoka kwa Rais wa nchi na wengine walikuwa wakipewa memo hizo kutoka kwa mawaziri mbalimbali.
"Hakuna ufisadi ambao umefanyika kwa bahati mbaya, hakuna ufisadi ambao umefanyika nchi hii pasipo waziri au aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujui. Hakuna ufisadi uliofanyika leo hii bila wakurugenzi kupewa vimemo ama kutoka kwa Rais, au kutoka kwa waziri wafanye maamuzi waliyofanya leo wanajifanya wanatumbua vijipu kumbe wanatumbua vipele, sababu wale walifanya kwa maelekezo ya wakubwa." Alisema Halima Mdee.

Katika hatua nyingine mbunge huyo wa Kawe amesema kuwa wao wanapozungumza leo hawazungumzi tu kwa sababu ya Chadema na UKAWA bali wanazungumza kwa maslahi mapana ya watanzania walio wengi ambao maisha yao ni magumu yaani kifupi wamepigika.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90