Top Ad 728x90

Sunday 21 February 2016

Kisiasa Zaidi............Kutoka Uganda..Huyu Ndio Aliyetangazwa Rasmi na Tume ya Uchaguzi Kuwa Mshindi wa Urais

Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali
yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa na Yoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986 ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.

Kituo cha TV cha NBS kimeripoti kwamba huduma za Taxi mitaani, mitandao ya kijamii na huduma za benki za simu za mkononi zimerejea baada ya serikali kuamuru juzi kila kitu kizimwe kuanzia Facebook, Twitter, Whatsapp.

Rais Museveni baadae alihojiwa na kusema mitandao ya kijamii ilizimwa kwa muda mfupi tu na watu hawakutakiwa kuwa na hofu sababu ilifanywa ili kuzuia upotoshaji wa taarifa tu ambao umekua ukifanywa mara kwa mara.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90