Top Ad 728x90

Wednesday 24 February 2016

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA YA KUUNGANISHIWA MAJI.


RYALO
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limefanikiwa kuunganishia huduma ya maji jumla ya wateja wapatao 183,500 wakiwemo wateja wapya 3500.
Shirika hilo bado linaendelea kupokea maombi mapya ya kuunganishia maji wateja wapya ili kutatua kero inayowasumbua wakazi wa jiji la Dar es salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa DAWASCO, Evalistine Lyaro alipozungumza na MAELEZO  ili kupata ufafanuzi wa namna shirika hilo lilivyojipanga katika kuwaunganishia maji wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo Mkoani Pwani.
 “Shirika limepunguza viwango vya maunganisho mapya ambapo kwa sasa mwananchi atalipia kiasi cha Sh. 200,000 na kupata huduma ya maji kwa muda mfupi na kwa wale ambao wapo zaidi ya umbali wa mita 50 watachangia gharama kidogo ya vifaa ili waweze kuunganishiwa maji” Evalistine.
Wananchi wote wa maeneo hayo wanatakiwa kuomba kupatiwa huduma hiyo kwenye ofisi yoyote ya DAWASCO iliyo karibu nao au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba022-2194800 au 0800110064 ambapo huduma hiyo ni ya bure.
Zoezi hilo la kuwaunganishia maji wateja wapya linafuatia kutekeleza agizo la Serikali la kuwafikia wateja Milion Moja katika mwaka huu wa fedha 2015/2016 ambalo limeanza rasmi Januari 01, 2016 na limegawanyika katika awamu kuu nne.
Awamu ya kwanza ya kuwaunganishia maji wateja hao itawahusisha wateja wote walioko katika maeneo ambayo kwa sasa yanapata maji na kuna miundo mbinu ya mabomba karibu, awamu ya pili itahusu maeneo ambayo yamepitiwa na mabomba makubwa ya maji jirani lakini wananchi wake hawana maji kwa sababu ya kukosekana kwa miundo mbinu ya usambazaji.
Wakati awamu ya tatu itahusisha maeneo yote yaliyopitiwa na mradi maarufu wa mabomba ya Kichina, Maunganisho katika awamu hii yataanza baada ya kukamilika kwa Miradi ya Ruvu Chini na Ruvu Juu na awamu ya nne itaanza katika maeneo yote ambayo kwa sasa hakuna miundo mbinu ya Maji na yako mbali kutoka katika mabomba makubwa.
Aidha, wananchi wote wa maeneo hayo wanahamashishwa kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa maji ili waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuhakikisha wanapata maji safi waweze kupambana na magojwa mbalimbali ambayo ni adui mojawapo wa taifa.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90