Top Ad 728x90

Monday 22 February 2016

Waziri Mbarawa Ampa Wiki Moja Mkandarasi wa Korea Kutoa Mikataba kwa Watanzania


Waziri wa ujenzi Makame Mbarawa ametoa wiki moja kwa mkandarasi anayetengeneza barabara ya njia nne kutoka Sakina hadi Tengeru mkoani Arusha kuhakikisha anatoa mikataba kwa wafanyakazi wa kitanzania wanaofanya kazi bila mikataka na akishindwa kufanya hivyo serikali itafuta mkabata wake kumshitaki na kumfukuza nchini.

Waziri Makame Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa kumi na nne nukuta moja inayo jengwa na kampuni ya Hanil-Jiangsu kutoka nchini Korea ambapo alipata malalamiko ya wafanyakazi wa kitanzania kufanyishwa kazi bila mikataba huku wakipata manyayaso kutoka kwa mkandarasi huyo.



Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Arusha John Kalupale amesema ujenzi wa barabara hiyo unakabiliwa na changamoto nyingi zilizosababisha kuchelewa kwa utekelezaji wake kwani hadi sasa ni asilimia saba tu ya ujenzi uliyofanyika na imebaki miezi tisa muda uliyo pangwa kumaliza.



Meneja wa miradi kutoka Tanrods makao makuu Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema katika shilingi bilioni ishirini za kulipa fidia kwa watu wanaondolewa kupisha ujenzi huo tayari bilioni nne zimeshapatikana na hakuna mtu atayeondoshwa kwenye eneo lake bila kulipwa fidia.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90