Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari
leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutengua
uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji mkuu wa baraza ilo Bw. Henry
Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar es Salaam kutokana utendaji
usiolizisha.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati
alipotembelea ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo hii kuona
utendaji wa Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
la Taifa Bw.Dionis Malinzi(kulia) akiongea jambo na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye.
Picha na Daudi Manongi.
……………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza
wajibu wake.
Mhe. Nnauye alitengua uteuzi huo
katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona
miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.
“Baraza likirekebishwa vyama vya
michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika
michezo,”alisema Mhe. Nnauye.
Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka
saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani
hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu
alipoteuliwa mwaka 2009.
Kutokana na utenguzi huo Mhe.
Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la
Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya
BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.
Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka
mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na
mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo
nchini.
Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza
Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia
Lihaya kazi nyingine wizarani.
0 comments:
Post a Comment