Top Ad 728x90

Thursday 18 February 2016

Dogo Janja Aikana Sauti yake Akimtongoza Msichana na Kuwaponda Tip Top...Madee Amtetea Asema Utoto Unamsumbua...

Rapper Dogo Janja ambaye kwa sasa yuko chini ya uongozi wa Tip Top  ameikana sauti iliyosambaa mitandaoni inayodaiwa kuwa ni yake akiwa anamtongoza msichana na kusikika akiu diss uongozi wa Tip Top kuwa unambania(soma hapa)

Dogo Janja alipoulizwa na kituo kimoja cha redio kuhusiana na sauti hiyo alikataa na kusema hajui chochote kuhusiana na swala hilo mpaka afuatilie.

Hata hivyo Madee alipoulizwa kuhusiana na sauti hiyo akasema ameisikia lakini ameigundua ni mambo ya kitoto ya dogo Janja pengine aonekane ana sauti kwa huyo binti aliyekuwa anamtongoza.

“Nimesikiliza nimeona mambo ya kitototo ndo maana hata sijataka kuhangaika nayo sana,nilichogundua ni kwamba alitaka kujionyesha anaweza kuongea kwa sauti yoyote kwa mwanamke lakini kama Tip Top tutakaa tutajua nini cha kumwambia” alifunguka Madee na kuweka wazi kuwa ngoma mpya ya dogo Janja itatoka mwisho wa mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90