Akizungumza na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita, Buguruni, Wilaya ya Ilala, Issa Mohamed, mume wa Upa alisema kwamba mkewe kwa sasa anaendelea vizuri ukilinganisha na mara ya kwanza alipofikishwa hospitalini hapo baada ya kupatikana katika bonde la Mto Msimbazi maeneo ya Tabata, Januari 23, mwaka huu.
‘Msukule’ wa tajiri aendelea vizuriAidha, Mohamed aliendelea kusema kwamba Upa yupo Muhimbili katika kitengo cha watu wenye matatizo ya akili anakofanyiwa uchunguzi na matibabu na kwamba amekuwa akienda kumjulia hali na kumpelekea chakula ambapo hata yeye amekuwa akijisikia vizuri anapomuona mumewe, jambo ambalo linamfanya wale naye pamoja, kuzungumza kisha kuagana.
“Kwa mara ya kwanza alipopatikana katika shimo nyumbani kwa tajiri na kutoweka akiwa mikononi mwa polisi kisha kupatikana tena kwenye bonde la Mto Msimbazi, kuna tofauti kubwa. Namuombea kwa Mungu apone haraka arudi nyumbani kwani watoto wamekuwa wakimlilia,” alisema Mohamed.
Upa aliaga nyumbani kwa dada yake mkubwa anayeishi Tabata Matumbi, Dar mwanzoni mwa mwezi Januari, mwaka huu akidai anakwenda kuwanunulia nguo wanaye katika Soko la Buguruni lakini hakurudi nyumbani ambapo baadaye alipatikana katika shimo, nyumbani kwa Mtei.
Global Publishers
0 comments:
Post a Comment