Top Ad 728x90

Sunday 5 October 2014

CHADEMA Mwanza yajipanga kuikabili CCM


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Mwanza kimeandaa mbinu  za kukiangamiza Chama Cha
Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Kiongozi wa operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema kuwa, hawatasita kuwaeleza wananchi vitendo wanavyovifanya baadhi ya wabunge wa CCM.
Alisema CCM imekuwa ikishindwa kusikiliza na kutambua matatizo yanayolikabili taifa, badala yake wamekuwa wakitumia nyadhifa zao vibaya kuihujumu nchi, kitendo kinachosababisha kuendelea kuwa masikini.
Njugu, alisema baadhi ya wabunge wanaotokana na CCM, wamekuwa wakishindwa kujadili mawazo ya wananchi kama yalivyokusanywa wakati wa mchakao wa kujadili rasimu ya katiba na kuweka kile watanzania walichokusudia kukipata.
“Tutawatumia walimu, wanafunzi na watumishi wa sekta ya umma kuhakisha watanzania wanapata katiba iliyo bora, hatuwezi kunyanyaswa na sisi tunaangalia, kuna baadhi ya vigogo wa CCM wanaona ile rasimu iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba inawabana ndo maana wanadiriki kupitisha mambo ambayo hayakuwemo,” alisema.

0 comments:

Post a Comment

Top Ad 728x90