Top Ad 728x90

Saturday, 27 February 2016

Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access....Yaua Mlinzi na Kupora Pesa, Polisi Wapambana Nayo na Kuyaua

by

Majambazi  ambao  idadi  yao  haikufahamika  wakiwa  na  mabomu  na  bunduki  za  kisasa  jana  walivamia  Benki  ya  Access  tawi  la Mbagala  ambako  walipora  viroba vya   fedha, kuua  mlinzi  na  baadae wanne  kati  yao  waliuawa  na  jeshi  la  polisi.

Watu  walioshuhudia  tukio  hilo  walisema  baada  ya  majambazi  hao  kufika  katika  benki  hiyo  kwa  bodaboda  nne  majira  ya saa  nane  mchana,yalimuua  mlinzi  wa  benki  hiyo, kusha  kubomoa  kwa  risasi  mlango  wa  vioo  na  kuingia  ndani  na  kuzua taharuki  kubwa

Mashuhuda  hao  walisema, katika  tukio  hilo  lililodumu  kwa  karibu saa  moja,mmoja  wa  majambazi  hao  aliyekuwa  amevaa  kininja,alikuwa barabarani  akiamuru  magari  kupita  haraka  huku  akifyatua  risasi  hovyo.

Ilielezwa  kuwa, jambazi  huyo  aliyeonekana  kuwa  na  uzoefu  wa  matumizi  ya  bunduki  alikuwa  akifyatua  risasi  kwa  kutumia  mkono  mmoja  na  ndiye  aliyewajeruhi  baadhi  ya  wapita  njia.

Hivyo,wakati  uporaji  ukiendelea  na  jambazi  huyo  akiimarisha  ulinzi  barabarani  baadae  hakukuwa  na  magari  wala  pikipiki  zilizokuwa  zikipita.

Mfanyabiashara  wa  duka  la  vifaa  vya  ujenzi  jirani  na  benki  hiyo,Ramadhani Tairo  alisema  baada  ya  jambazi  huyo  kuliona  gari  la  polisi  likielekea  eneo  la  tukio,alifyatua  risasi  na kulipiga  kabla  halijafika.Gari  hilo  lilipoteza  mwelekeo  na  kutumbukia  mtaroni.

Tairo  alisema  mbali  na  jambazi  huyo  kulipiga  risasi  gari  la polisi  pia  alilirushia  bomu  la  mkono,lakini  liliangukia  barabarani  bila  kuripuka.Polisi  walifanikiwa  kulilipua  bomu  hilo  baadae  likiwa  halijasababisha  madhara  kwa wananchi  waliofika  kushuhudia  tukio  hilo.

Mkazi  mwingine  wa  eneo  hilo,Rebecca  Maliva  alisema  majambazi  walioingia  ndani  ya  benki  hiyo  walioneka  wakitoka  na  viroba  vitatu vya  fedha  ambavyo  walivipakata kwenye  pikipiki  na  kuondoka  kwa  kasi  kuelekea  Mkuranga kupitia  barabara  ya  Kilwa.

Rebecca  alisema  polisi  zaidi  walifika  kwenye  eneo  hilo  wengine  wakiwa  kwenye  pikipiki  na  kuanza  kuwafukuza  majambazi  hao  ambapo  walipofika  eneo  la  shule  ya  St. Marry's,walitupa  kiroba  kimoja  cha  fedha  ambacho  wananchi  waliokuwa    jirani  waligombania  na  kuchukua  fedha  zilizokuwemo  na   kisha  kila  mmoja  kukimbia  na  burungutu  la  noti.

Baada  ya  nusu  saa  wakati  umati  ukiwa  bado  upo  kwenye  benki  hiyo,magari  ya  polisi  yalipita  katika eneo  hilo  yakitokea  eneo  la  Mkuranga  yakiwa  yamebeba  miili  ya  majambazi  yaliyouawa.

Magari  hayo  yalikuwa  yakisindikizwa  na  vijana  wa  bodaboda  waliokuwa  wakishangilia  kazi  iliyofanywa  na  polisi.

Kamanda  wa  polisi  kanda  maalum ya  Dar es Salaam, Simon Sirro  alizungumzia  kwa  ufupi  tukio  hilo n kwamba  majambazi  manne  yaliuawa  na  kukamata  silaha  tatu,lakini  hakutaka  kuingia  kwa  ndani  akisema  atatoa  taarifa  zaidi  leo

Msanii Rich Movoko Amkana Mrembo Gigy Money 'Sikumbuki Hata Kukutana na Gigy Money Wala Kutoka Nae Kimapenzi Sinaga Upumbavu Huo

by

 Gigy Money na Rich Mavoko....
Msanii Rich Mavoko amekanusha taarifa za kuwahi kuwa na mahusiano na video queen Gigy Money, ambaye alisema alishawahi kuwa naye akiwa kidato cha pili.

Akiongea na East Africa Radio Mavoko amesema taarifa hizo si za kweli, na hakumbuki hata kuwahi kukutana naye mrembo huyo, achilia mbali kuwa na mahusiano naye.
“Mi sijawahi kutoka naye, hata siku moja sijawahi, sina urafiki naye na wala sijawahi kuongea naye, sijui kama alishawahi kukutana na mimi, sijaweka kichwani kama nishawahi kukutana nae sikumbuki.

Mavoko ameendelea kusema "Sijawahi kuwa na skendo za kipumbavu, mi ni mtu ambaye sijawahi kuwa na upumbavu kama huo, kwanza mi mwenyewe nashangaa unajua kila kitu, sijawahi kutoka naye sijui mwenyewe anafikiria nini, siwezi kujua, siwezi kutambua, sijawahi kuelewa nini kilichompelekea hivyo”, alisema Richi Mavoko.

Hivi Karibuni video queen huyo alisema alishawahi kuwa na mahusiano na msanii huyo wakati yupo kidato cha pili, kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi na hakifai kwa mtu ambaye ni kioo cha jamii.

Staa wa muziki Mzungu Kichaa Awadiss Wema Sepetu na Idris Sultan

by

Mzungu Kichaa
Staa wa muziki Mzungu Kichaa, amevunja ukimya kuligusia suala ambalo pengine linawaumiza wasanii wengi, ikionekana kuwa ni 'diss' pia kwa staa Wema Sepetu na mwenzake Idriss Sultan, kupitia suala lao la ujauzito kunasa na kutoka.

Akiongea kwa hisia nzito, Mzungu Kichaa ambaye ana project kubwa ya video ambayo watu hawaifahamu kama wanavyofahamu mimba ya Wema, msanii huyo anayejinadi kuwa ni mbishi, ameelezea kusikitishwa kwake kwa mastaa hao ambao wanatumia muda wao mwingi kuleta atensheni kwa mashabiki badala kufanya shughuli zao binafsi za kila siku.
Idriss na Wema Sepetu

Mzungu Kichaa pia amekanusha suala la video yake kukosa kiki kutokana na kumhusisha Dir Adam Juma ndani yake, na kuifanyia hapa hapa nchini akisema kuwa Dir Adam ana kila sababu ya kupewa hashima yake kutokana na ubora wa kazi zake na si maelezo mengine yaliyopotofu.

Kama Ulikuwa Unafikiri Mr Nice Kafulia Basi Umechemsha..Adai Bado ana Hela Alizovuna Kipindi cha Nyuma Katika Muziki Wake

by

Msanii mkongwe na mwanzilishi ya style ya TAKEU, Mr Nice amefunguka kwa kusema kuwa bado yupo vizuri kiuchumi tofauti na watu wanavyodhani kwamba amefilisika.


Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Mr Nice amesema kwa kuthibitisha hilo amejenga nyumba mpya kubwa nyumbani kwao ndani ya miezi mitatu.

“Watu hawajui kwamba walinipa pesa nyingi sana mpaka leo bado nazitumia, nyie mnaona kama zimeisha hazijaishi, hapa sasa hivi nawazima kidomo domo wale waliosema nimefilisika, sasa hivi najenga nyumba nyingine kijijini kwangu Moshi na ndani ya miezi mitatu nyumba kubwa imekamilika,” alisema Mr Nice.

Aliongeza, “Watu ambao umefilisika watafikiria kujenga sasa hivi?, hamuwaoni wasanii wenye stress za maisha, kwa hiyo hili ni jibu kwa wale waliyokuwa wanaongea sana,”

Nay wa Mitego Avunjiwa Kioo Cha Gari yake..Alikuwa Anaenda Kutambulisha Video ya Shika Adabu yako

by

Rapper Nay wa Mitego amekutwa na misukosuko ya kuvunjiwa kioo cha gari lake na watu wasiofahamika wakati anaenda kutambulisha video yake mpya ya shika adabu yako kwenye kipindi cha FNL cha EATV.

Kupitia akaunti yake ya instagram @NayTrueboy rapper huyo ameweka picha ya gari hiyo ikiwa imevunja kioo na kuandika maneno yafuatayo..

”Nimevunjiwa kioo Cha gari nikiwa njia naenda kwenye Intrvw Chanel5 EaTv kwa ajili ya kutambulisha my New Video #ShikaAdabuYako sorry Watu wangu mliokua mkisubiri kuona Video Na Interview yote nimeshindwa kufika naweka sawa ili. Video itaenda YouTube kesho itakua kwenye Tv yako Pendwa. Muziki sio vita….. I will never stop doing what i do.!!“

Maskini Jamaa Auawa Baada ya Mpenzi Wake Kumwita Mwizi Chuo cha SAUT Mwanza..Alikuta Message za Mwanaume Mwingine Kwenye Simu ya Mpenzi wake

by

Kwa masikitiko makubwa tukio tajwa hapo chini limetokea Chuo cha SAUT Mwanza ambapo Jamaa wa jinsia ya kiume ,alienda kumtembelea mpenzi wake chuoni SAUT bweni la RUGAMBWA,

Ukweli ni kwamba huyo jamaa na huyo demu ni wapenzi wa muda mrefu na pia jamaa sio mwanafunzi ni raia wa kawaida anayehusika na mambo hasa ya modeling na amekuwa akiandaa event mbalimbali kama mtakuwa na kumbukumbu vizuri kuna kipindi kulitokeaga shindano la MISS ALBINISM lililofanyika Mwanza huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wahusika wa hilo shindano,na siku tatu zilizopita huyu jamaa alitoka kumzika baba yake mzazi.

Kilichotokea hapo ni baada ya jamaa kwenda hosteli za wanawake ambazo zipo ndani ya chuo ambapo ndipo alipokuwa akiishi huyo demu wake, katika kukagua simu ndipo akakuta sms za utata, ukatokea ugomvi katika mabishano demu akasema atamwita mwizi kama utani kweli demu akaita mwizi.

Jamaa kwa kuogopa na sababu hakuwa na kitambulisho ndipo akatoka mbio, hapo ndipo alipoharibu wananzengo na wanachuo bila kujali wakaanza kupiga na mpaka wanafika polisi alikuwa kapigwa sana, alipelekwa kituoni kutoa maelezo. Baada ya hapo ndipo tukapata taarifa kafariki na hiyo ni sababu ya kipigo.

Picha ya Roma na Mdogo wa Kike wa Ali Kiba ilivyozua Utata..Imekuaje?

by

A
Ikiwa zimesalia wiki kadhaa ili msanii wa Hip Hop Tanzania,Roma kufunga ndoa na mpenzi wake anayejulikana kama Nancy au Mama Ivan kumeibuka na utata baada ya kusambaa kwa picha ya msanii huyo akiwa kwenye pozi linaloonekana ni la kimahaba na zabibu Kiba,mdogo wa kike wa Ali Kiba na watu kuhisi huenda wawili hao wakawa wana mahusiano ya kimapenzi

Kituo cha redio kimoja kilimtafuta mke mtarajiwa wa Roma na kumuuliza kuhusiana na picha hiyo ambapo bibie huyo alidai kuwa hajui chochote na wala hajali kwani inaweza ikawa picha tu na shabiki na kuongeza kuwa Roma hawezi kufanya upuuzi.

Kwa upande wake Roma alipotafutwa alionekana mwenye kusita sita na kutaka kujua kama mazungumzo hayo yapo On air au Off Air,baadaye Roma alikiri kuwepo kwa picha hiyo na kudai ni ya kitambo na hakumbuki ilikuaje kwenye picha hiyo na kuomba aulizwe zaidi kuhusiana na kazi za muziki kuliko mambo mengine ya nje.

Top Ad 728x90