Top Ad 728x90

More Stories

Sunday 6 March 2016

Mange Kimambi Afunguka Baada ya Mtaliano Kuandika Barua ya Kuwashafisha January na Mwamvita Makamba....

by





"Mangekimambi_ hii ndio Tanzania yetu. Mlalamikaji ambae a few hrs before aliingia Twitter Na kumtishia January Kuwa atae expose na Safari Yao ya Dubai amesainishwa na barua na wana sheria kabisaa ya kumsafisha January Makamba! . .

Have you guys seen anything like this before?? Does it make sense?? a few hrs before mlalamikaji anatoa vitisho hadharani then anafanya a complete 100% turn around , akili kichwani kwako Mtanzania! Wow! Anyways, like I said any reasonable average person anaelewa what happened, you don't need to be a genius. Yani hata Waziri Mkuu na Rais wakiamua kumwacha January ni vile waamue but from zile audio za Mwamvita, to interview ya January hata wao wanajua January is guilty as charged!

Barua yenyewe wamemuandikisha fasta Mpaka wamekosea date

Hata wasipomchukulia hatua Ila In 2020 we will not forget , voice note bado zitakuwepo, email bado zitakuwepo, interview ya January bado itskuwepo Na tutawakumbusha Watanzania " Mange

Rais Magufuli Ampiga Chini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.....John Kijazi Kateuliwa Kuchukua Nafasi Yake

by


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. 

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi  wa Mawasiliano,
 IKULU-Dar es Salaam
06March,201
Katibu Mkuu Kiongozi Mpya, Balozi John William Kijazi

Ushindi wa Lulu na Richie kwenye AMVCA 2016 utaziongezea pumzi filamu za Kibongo

by
Tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards, ni sawa na Oscars za Afrika. Ndiyo tuzo kubwa zaidi zinazoikutanisha tasnia ya filamu Afrika nzima pamoja.

Utofauti kati ya tuzo za Oscars na AMVCA ni kuwa tuzo za Oscar zinaikutanisha industry ya filamu ya Marekani iliyounganika pamoja, Hollywood bali AMVCA ni tuzo zinazokutanisha industry ndogo ndogo za nchi za Afrika.

Na kwa kiasi kikubwa tuzo za AMVCA ambazo mwaka huu zimetolewa kwa mwaka wa nne zimetawaliwa na Nollywood na kwa mbali tasnia ya filamu ya Afrika Kusini. Kwa kuona hivyo, waandaji walitengeneza tuzo za kikanda na za lugha maalum. Ndiyo maana kuna tuzo ya filamu ya Kiswahili na ya Afrika Mashariki.

Kwa mwaka huu tuzo hizo zote zimekuja Tanzania, ambapo Single Mtambalike maarufu kama Richie ameshinda kipengele cha filamu ya Kiswahili kupitia Kitendawili. Elizabeth ‘Lulu’ Michael alishinda kipengele cha filamu bora ya Afrika Mashariki, kupitia Mapenzi.

Na tumeshuhudia wenyewe kuwa ushindi huu umeshangiliwa zaidi na kurejesha imani katika filamu zetu. Ushindi wa Lulu na Richie unatupa moyo wa kuamini katika kazi za wasanii wetu. Ushindi huu umekuja katika kipindi ambacho tasnia ya filamu ya Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa katika pande nyingi. Imeshuka kwenye mauzo na usambazaji kiasi ambacho wasambazaji wakubwa wamepunguza kasi ya kusambaza kazi kama zamani na kuwafanya waigizaji wengi kubaki na filamu zao mkononi wasijue namna ya kuzisambaza.

Ni kwasababu ni watanzania wachache wenye muamko wa kutoa fedha mfukoni na kununua filamu za nyumbani. Pengine kwasababu ya utandawazi ambapo tumekuwa ‘exposed’ na filamu bora kutoka Hollywood, imekuwa ngumu sana kuziamini filamu za nyumbani hasa tunapotaka kuzifananisha. Kuna sababu nyingi sana zinazochangia tuziweze kufikia hata asilimia 10 ya ubora wa filamu za wenzetu. Uchumi, teknolojia, ujuzi, elimu, utafutaji na unolewaji wa vipaji kwenye filamu na mambo mengine kibao yanaifanya tasnia yetu iendelee kudoda.

Lakini pengine kama tukiamua kuweka nguvu kwenye vitu vinavyowezekana kama vile kutengeneza filamu zenye story nzuri na zilizobeba uhalisia pamoja na uchaguzi mzuri wa wahusika watakaowasilisha maudhui kwa ufahasa, watanzania wanaweza kushawishika kuzinunua filamu za nyumbani. Inabidi filamu zianze kutengeneza mjadala kama ambavyo muziki wa Bongo Flava umefanikiwa. Kwamba Ray akitoa filamu yake, watu waijadili kwenye mitandao ya kijamii kama ambavyo Diamond au Alikiba na wasanii wengine wakiachia video zao.

Tukirudi kwenye ushindi wa Lulu na Richie kwenye AMVCA, naamini kuwa umepeleka ujumbe Afrika kuwa Tanzania ina kitu. Kama ambavyo kimuziki tunaonekana kuwa vizuri, ni kwa kushinda tuzo kama hizi kunawashtua watu wa pande zingine za Afrika kuwa kumbe nasi tumo.

Cha msingi ni wasanii wetu kuongeza spidi zaidi kwa kutengeneza filamu ambazo hata kama zitatajwa kuwania tuzo hizo, zisiishie tu kuwekwa kwenye vipengele maalum, bali pia kwenye vipengele vya jumla. Tunapenda kuona siku moja Lulu, Kajala, Wema Sepetu, Nisha au Shamsa Ford wanashindana kwenye tuzo moja na Genevieve Nnaji wa Nigeria au Yvonne Nelson wa Ghana.

Tunapenda kuona siku moja Ray, Richie, JB au Hemedy wanashindana kwenye tuzo moja na Ramsey Noah wa Nigeria au Van Vicker wa Ghana.

Mimi ninaamini kuwa ushindi wa Lulu na Richie kwenye AMVCA 2016 utaziongezea pumzi filamu za Kibongo

Wema, Kajala Acheni Utoto Bwana!

by


KWENU warembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja. Habari zenu binafsi? Bila shaka ni wazima wa afya na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Kitambo kidogo sijawaona lakini naamini pumzi ya bure mnaendelea kuivuta ndiyo maana nasikia matukio yenu kwenye vyombo vya habari.

Mkitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima. Namshukuru Mungu naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Mungu ni mwema sana, anaendelea kubariki kazi ya mikono yangu, namuomba yeye aendelee kunibariki zaidi na zaidi.

Dhumuni la kuwaandikia barua hii ni kutaka kuwakumbusha kwamba nyinyi kwa sasa ni watu wazima. Umri wenu unatosha kabisa kusema haufanani na yale matukio yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Mara kadhaa nimewahi kuwaambia, hata yale mashindano yenu ya kumwaga fedha ukumbini, nyakati hizi si zake.

Mambo ya kuibiana mabwana kama yalishatokea, itoshe sasa kusema ulikuwa ni ujana. Kwa kuwa ilitokea, hakuna namna zaidi ya kuyasahau na kuchapakazi. Soko lenu la filamu bado haliridhishi, lakini mnapaswa kukomaa ili angalau mtengeneze fedha kupitia kazi zenu na si kuhongwa.

Binafsi sikufurahishwa na tukio lenu la kukutana ukumbini na kuzinguana mbele ya kadamnasi lililoripotiwa wiki iliyopita na magazeti Pendwa. Lilikuwa tukio linaloonesha kwamba bado hamjakua kitu ambacho sitaki kukiamini.

Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, huu siyo wakati wa nyinyi kuoneshana ubabe wa fedha. Kwamba eti kwa kuwa mwenzako kaenda kutunza msanii jukwaani, na wewe lazima utunze nyingi zaidi ili uonekane wewe ni zaidi.

Ndugu zangu, bahati nzuri maisha  yetu tunajuana. Kwa kiasi kikubwa natambua maisha ya wasanii wetu nchini hususan warembo. Wengi wenu hamtegemei sanaa kuendesha maisha yenu. Wengi mnategemea  mapedeshee au ‘mabwana’ kutamba mjini.

Niwashauri hizo fedha mnazozipata ni bora mngewekeza kwenye sanaa yenu. Mkajizatiti vizuri ili ziweze kuzaliana. Mnapigana ili iweje? Mnatambiana mbele za watu inawasaidia nini. Wenzenu wanapigana siku hizi wanaingiza fedha.

Nyinyi kazi yenu si ubondia. Kazi yenu ni uigizaji. Igizeni kwelikweli na Watanzania wawaunge mkono kwa kununua kazi zenu. Sanaa yenu ina changamoto nyingi, mnawezaje kuzishughulikia ikiwa hamna umoja.

Mtawezaje kutatua changamoto hizo ikiwa hamna upendo kati yenu? Si rahisi kutatua changamoto hizo wakati mna chuki. Ili mfanikiwe, mnahitaji kushirikiana. Shirikianeni ili muweze kuisogeza sanaa mbele, acheni vita ya kipuuzi mnayoendelea kuifanya.

Mkizingatia hayo niliyowaambia, hakika tutaona mabadiliko kwenu na sanaa kwa ujumla. Nina imani nyinyi ni watu wazima na mtajipanga upya na mtaanza kuchapa kazi kama kauli mbiu ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ‘Hapa Kazi Tu’.

Ni mimi mtu wenu,

Erick Evarist.

GPL

Mbwana Samatta Aonja Machungu Kwa Mara ya Kwanza Kwenye Timu yake Mpya ya Genk..

by


Nyota wa Tanzania Mbwana Samatta na klabu yake ya Genk walitoka vichwa chini baada ya timu yao kuchapwa bao 2-1 na klabu ya Standard Liege kwenye mchezo wa ligi kuu ya Belgium uliochezwa usiku wa Jumamosi March 5.

Genk wakiwa ugenini ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 42 kipindi cha kwanza likifungwa na Nikolaos Karelis na kuipeleka Genk mapumziko ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0.

Dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza, Ivan Santini akaisawazishia Standard Liege kabla ya Jean-Luc Diarra Dompe kuifungia Standard bao la ushindi na kupeleka msiba kwa Genk.

Kama kawaida Samatta iliingia uwanjani dakika ya 81 kuchukua nafasi Karelis lakini bado haikutosha kubalili matokeo.

Samatta anaishuhudia klabu yake ya Genk ikipoteza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo mwezi January akitokea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemrasia Kongo.

Top Ad 728x90

Top Ad 728x90